NYOTA ZENU LEO JUMATANO TAREHE 16/2/2022
NDOO ( Jan 20- February 19)
Wiki hii inaonekana umekuwa mzito na Umesitasita kwa muda mrefu kufanya maamuzi. Usiogope jitoe muhanga iwapo unataka kufaulu hasa katika mambo yako.
SAMAKI ( February 20- March 20)
Utahitaji ushauri mzuri ili kuweka mambo yako sawa. Kutimia kwa mipango yako uliyonayo kunategeme wewe utajihusisha na mambo ya aina gani
PUNDA ( March 20-April 20)
Leo imekuwa vigumu kwako kufanya maamuzi kuhusiana na mambo Fulani na utajikuta uko njia panda itakayokutenganisha na mambo mengi. amua cha kufanya katika kufikia malengo yako unayoyataka.
NGOMBE( April 21- May 20)
Umekuwa ukisumbuliwa na mikosi na matatizo sasa kwa muda mrefu na leo ndio hasa wakati hasa wa kuyashughulikia hayo matatizo yako na kuyamaliza.
MAPACHA ( May 21- Juni 20)
Leo uwe na hisani kwa kila mtu na jitolee kutoa msaada, tabia hiyo itawafanya watu wakuthamini , ikiwezekamna mara kwa mara toa msaada kama unavyotoa kwa wengine na wakija wasaidie wala usichoke
KAA ( Juni 21- Julai 22)
Leo badilika na jiweke mbali na marafiki wabaya iwapo utataka kufaulu katika maisha yako. umekuwa ukitumia vibaya fedha zako kiasi cha kushindwa kutekeleza baadhi ya mambo yako ambayo umejipangia wewe mwenyewe, Acha hiyo tabia
SIMBA (Julai 22-Agosti 22)
Matatizo mengi ambayo yaliyokuandama yalikuwa yanatokana na mikosi kwa upande wako, Tafuta njia ya kuondoa husda hiyo au nuksi hizo kabla hazijakuletea madhara kwa sehemu kubwa kwako,
MASHUKE (Agosti 23-Sep 23)
Ondoa khofu. Nyota yako itakuletea mambo makubwa na mengi sana katika maisha yako. Yakitokea hayo yakubali tu hatimaye utamakinika na utaona faida ya mabadiliko hayo.
MIZANI ( Sep 23-Oktoba 23)
Leo tafuta ufumbuzi au utatuzi wa shida zako zinazokukabili. Jiepushe na marafiki wasio na tija kwako. Leo Unahitaji utulivu wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yako yanayokukabili.
NGE (Oktoba 23-Nov 22)
Leo ni Jumatano nzuri sana kwako hasa katika kubuni mbinu na Mipango ya maisha yako ya baadae, yaweke pembeni mambo ambayo unayaona hayana maana na simamia kile ambacho unakiamini
MSHALE (Nov 22- Desemba 21)
Leo tumia Jitihada binafsi kujielekeza kwa mambo mema unaweza kufanikiwa. Utakutana na mgeni na atakutaka muwe marafiki, mkubalie kwa sababu utapata faida kubwa kwa hilo hasa kwa wiki inayokuja.
MBUZI ( Desemba 21- Jan 20)
Siku ya leo Kuna bahati kubwa sana ipo upande wako ,watu wengi watakuchangamkia na watakuwa tayari kukusaidia kuyashughulikia matatizo yako yanayokukabili
No comments:
Post a Comment