Sunday, 5 August 2018

NYOTA YAKO LEO JUMAPILI

PUNDA

Tegemea kupokea habari njema na mambo ya kukufurahisha pia kuna mtu mliepotezana muda mrefu atakutafuta au mtakutana pia jiepushe na uongo siku ya leo sio mzuri kwa kudanganya unaweza kuumbuka.

NG'OMBE

Leo utapata ugeni mkubwa na kuna watu watakutembelea,pia tegemea kujifunza jambo, huu ni msimu mzuri kwako kimahusiana na mahusiano ila sio wakati mzuri kipesa na kiuchumi ni wakati mgumu kwako waone wataalam  kujua tatizo lilipo.

MAPACHA

Safari zako zina kheri kubwa jitahidi uende, pia kuwa muangalifu na mambo yako unayoyafanya kuna watu wanakufuatilia ili kukuvurugia mipango yako ni vyema kuzingatia kuwahi kurudi nyumbani leo kwani jioni sio muda mzuri kwako.

KAA

Kuwa makini na mali zako unaweza kuibiwa au kupoteza kitu muhimu, pia tegemea faraja kwa mtu unaeenda kukutana nae leo au kesho pia kuwa huru na mambo yako.

SIMBA

Mambo yako unayoyafuatilia yatatimia bila shaka yoyote ugumu ulioupata mwanzo usikufanye ukwame juu ya kile unachokifuatilia ongeza juhudi utafanikiwa ila tabia yako ya kutumia nguvu au hasira ili kutimiza haja yako itakukwamisha jitahidi kubadilika.

MASHUKE

Mambo yako leo yatakuwa magumu na jitahidi kumtanguliza mungu ikiwa una safari au jambo lolote unalifuatilia kutakuwa na uzito pia leo usiingie mkataba au makubaliano yoyote utasalitiwa.

MIZANI

Afya yako au ya mgonjwa wako itakuwa vizuri na utapata matumaini pongezi na shukran kwa kile ulichokifanya, siku ya leo jielezee shida yako kwa mtu atakusaidia.

NG'E

Maswala ya kipesa sio mazuri kwako siku ya leo kutakuwa na uzito juu ya unachokifuatilia, Pia jihadhari na maamuzi yako yanaweza kukutia hasarani.

MSHALE

Uliyegombana nae atakutafuta leo au ndani ya wiki hii na ugomvi utaisha au utatoweka Pia tumia muda ulionao kuyafuta.

MBUZI

Leo mambo yako ya kimahusiano yataenda vizuri pia utapokea lawama zisizo na mantiki Ikiwa una safari yoyote basi itimize usiiahirishe utapoteza vitu muhimu kwako.

NDOO

Migogoro kazini au katika ndoa yako itazidi kuwepo jitahidi kupunguza marafiki pia usiamini sana unachoambiwa amini unachokiona pia kuna jambo kubwa na zuri atakalolifanya mwenzako tegemea faraja.

SAMAKI

Mambo yako ya safari ulizozipanga yatatimia na kwenda vizuri pia kuna jambo baya analolifanya rafiki yako kama unavyomuotea ni kweli sio mtu mzuri sana kwako fuatilia na uchukue maamuzi.

Usikose masomo ya utabiri kila siku hapa kwenye website yetu asiye jua nyota yake atoe tarehe ya kuzaliwa

Asiye na tarehe ya kuzaliwa atachangia sh.5000/= na utapatiwa maelekezo.

Maalim Mambikhi
+255 745 59 50 89

No comments:

Post a Comment