Monday 6 August 2018

NYOTA

UTABIRI WA LEO JUMATATU

Punda(21 march-20 april)

Siku ya leo tegemea kukwaruzana na mtu kwa vitu vidogo visivyo vya msingi hali hii imeanza usiku wa jana na itaendelea hadi leo usiku, Kuwa huru na ujiamini kwa kila ufanyalo kikubwa usivuke mipaka katika kujiamini.

Ng'ombe(21 april-21 may)

Siku ya leo mambo yako yataanza kukufungukia na kutimia leo tegemea habari njema kutoka usipopatarajia pia utakumbukwa na marafiki waliokusahau na mahusiano yatazidi kuwa vizuri pia kuna dalili ya safari nenda safari yakk ina kheri.

Mapacha(22 may-21 may)

Siku ya leo kuwa makini na safari uliyoipanga utaudhiwa na kukerwa pia watu hawatothamini muda wako fanya mawasiliano kabla ya kutoka, Pia kuna fitna inayofanywa ili ugombane na mwenzako jihadhari na ujiimarishe zaidi usijisahau kiibada.

Kaa(22 june-22 july)

Leo ni siku nzuri kwaako maradhi yatakwisha unaonekana kusumbuliwa san na tumbo hali hiyo itaisha, pia tegemea kupata mazuri uendapo na kuna dalili za kuahidiwa kitu kikubwa na kitu hicho kitatimia.

Simba(23 july-21 august)

Leo ni bora kutulia nyumbani kuna mtu amepanga njama mbaya juu yako, mtu huyu ni rafiki wa mtu wako wa karibu jihadhari na jambo na ununue kibiriti upele nuia kisitokee chochote jivu litakalotoka hapo lifunge na ulitupe chooni.

Mashuke(22 august-22 september)

Afya yako itaenda vizuri kama una mgonjwa basi hali yake itabadilika na kuwa nzuri, pia tegemea kupata matumaini makubwa katika shughuli yako uliyoipanga au jambo unalolifuatilia.

Mizani(23 september-21 october)

Leo utapata ugumu kipesa watafute wote unaowadai jitahidi kuwakumbusha, siku ya leo kuwa mpole zaidi.

Ng'e(22 october-21 november)

Jitahidi kuwa makini na ulaji na unywaji wako unaweza kusumbuliwa na mafua homa homa hali hii ni ya mpito tu pia migogoro uliyo nayo itafikia ukomo.

Mshale(22 november-21 december)

Leo utadanganywa au kuongopewa kitu na utaujua ukweli baadae, pia kuwa makini leo sio siku nzuri kimahusiano kwako .

Mbuzi(22 dec-19 january)

Leo usijihusishe na mkutano  au mikusanyiko ya watu wengi, na ikiwa kuna kikao hudhuria ila usiwe muongeaji utapingwa na kupuuzwa siku ya leo haifai kwako kwa kuomba msaada hutasaidiwa ils kwa shida shida.

Ndoo(20 january-18 february)

Tegemea kupokea habari njema siku ya leo kuna kitu utajifunza na kuna vitu vitakufurahisha.

Samaki(19 february-20 march)

Utapoteza kitu muhimu jitahidi kurudi nyumbani mapema siku ya leo pia toa sadaka kuondoa uzito katika mambo yako, Pia kuwa mkali katika mali zako haswa kwa wanaozitumia vibaya.

Usikose kuuliza swali na kufuatilia jibu la swali lako hapa

Kwa maswali ya siri utanipigia simu
+255 745 59 50 89

No comments:

Post a Comment